SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MADAKTARI KUANDIKA DAWA KWA MAJINA YA KAMPUNI

Serikali imepiga marufuku madaktari kuwaandikia wagonjwa dawa kwa kutumia majina ya kampuni badala yake watumie majina ya kitaalamu.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Oktoba 10, na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile, katika kuangalia mfumo wa upatikanaji dawa na vifaa tiba nchini.

Amesema tabia ya madaktari kuandika dawa kwa kutumia majina hayo ya kampuni kumesababisha wagonjwa kukosa dawa na licha ya kuwapo kwa dawa nyingine zenye uwezo wa kutibu sawa na hizo.


“Dawa zinazotumika hapa nchini ni sawa na zile zinazotumika katika nchi nyingine duniani, kwa hiyo kutoa dawa China, India, Marekani au Ulaya ni utofauti wa gharama.


“Kwa mfano mimi ni daktari nikikuandikia ukanunue soda ukikuta soda yoyote utapona ila nikikwambia ukanunue Cocacola lazima uipate hiyo.


“Kwa hiyo wawaAndikie wagonjwa dawa kwa majina ya asili kwa sababu ukimwandikia mgonjwa panadol ni kumtaka lazima anunue dawa hiyo hata kama kuna dawa nyingine hawezi kupewa,” amesema Dk. Ndugulile.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post