RIPOTI YA BENKI YA DUNIA: UCHUMI WA AFRIKA UNAPOROMOKA

Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia kwa Afrika, Albert Zeufack 
****
Benki ya Dunia imepunguza matarajio ya ukuaji wa uchumi kwa eneo la Afrika, chini ya jangwa la Sahara mwaka 2018 hadi asilimia 2.7 badala ya utabiri wa awali wa asilimia 3.1.

Kwa kiasi kikubwa hali hiyo inatokana na ukuaji wa pole pole wa uchumi katika bara hilo, kwa mujibu wa taarifa ya benki hiyo juzi Jumatano.

Eneo hilo, ambalo lilikuwa na ukuaji wa viwango vya wastani vya uchumi miaka kadhaa kuelekea mwaka 2015, ilipata hasara kubwa katika kasi ya ukuaji wake baada ya bei za bidhaa kushuka mwaka 2015 – 2016.

Mwezi Aprili, Benki ya Dunia ilibashiri kwamba ukuaji huenda ungekuwa kwa kasi zaidi mwaka 2018, ukuaji wa wastani ukiwa katika kiwango cha asilimia 3.1, ikiwa ni juu kutoka ukuaji wa asilimia 2.3 mwaka 2017.

“Kasi ya ukuaji wa pole pole barani Afrika chini ya jangwa la Sahara, unaelezewa kuwa unatokana na upanuzi usiotabirika wa kiuchumi katika mataifa matatu yenye uchumi mzuri ya Nigeria, Angola na Afrika Kusini,” taarifa ya benki imesema.

Kushuka kwa uzalishaji mafuta nchini Angola na Nigeria kumesababisha kupanda kwa bei za mafuta na nchini Afrika Kusini, ukuaji dhaifu wa matumizi ya majumbani kumetokana na kupungua kwa shughuli za kilimo, taarifa ya Benki ya Dunia imesema.

Nchi zingine katika bara hilo zimekuwa na ukuaji usiotetereka mwaka 2018, zikiwamo zile ambazo hazitegemei bidhaa, kama vile Ivory Coast, Kenya na Rwanda, benki imeongezeka kusema.

Albert Zeufack, mchumi mkuu kwa Afrika katika Benki ya Dunia, amezisihi serikali katika eneo hilo kuacha kutumia fedha vibaya na badala yake kuboresha uzalishaji ili kusaidia katika harakati za kufufua uchumi.

Madeni makubwa ya umma katika baadhi ya nchi kwenye bara hilo, ukichanganya na sarafu dhaifu na kupanda kwa viwango vya riba, huenda kukahatarisha uwezo wa kulipa madeni yao, Benki ya Dunia imeonya.

“Watunga sera katika eneo hilo lazima wajiweke sawa kukabiliana na hatari mpya ambazo zinajitokeza kutokana na mabadiliko katika mtiririko wa mitaji na madeni,” Zuefack anaesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527