MAKONDA APOKEA SMS KIBAO KUHUSU MASHOGA DAR

Ikiwa ni siku moja toka Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda atangaze kampeni ya kuanza kuwakamata mashoga pamoja na malaya ambao wanajiuza kupitia mitandao ya kijamii, ameanza kupata mrejesho.

Hatua hiyo imekuja baada ya msanii wa muziki, Amber Rutty kuachia video chafu mtandaoni hali ambayo ilimfanya mkuu huyo kutoa tamko la kutaka akamatwe.

RC Makonda alisema kwa tukio ambalo amelifanya msichana huyo anapaswa kufungwa jela, kwani ni ukiukwaji wa sheria za nchi huku akiwataka Wanadar es salaam kumtumia majina ya mashoga pamoja na watu ambao wanafanya biashara ya ngono mtandaoni.

“Nimepokea msg zaidi 5,763 na majina ya Mashoga zaidi ya 100 hii inaonyesha Wana DSM hawataki laana ya mashonga. Naendelea kupokea majina ya Mashoga,” amesema RC Makonda kupitia taarifa aliyoitoa siku ya leo.

Mkuu huyo amesema msako mkali wa kamata kamata ya mashoga na watu wanaojiuza utaanza wiki ijayo kwani kwa sasa anakiandaa kikosi kazi pamoja na kupokea baadhi ya majina.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post