ADAKWA GESTI AKITAPELI KWA KUJIFANYA AFISA USALAMA WA TAIFA KUTOKA IKULU


Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Richard Elieza Malisela (23) anashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa kosa la kujifanya Afisa Usalama wa Taifa kutoka Ikulu jijini Dar es salam na kujipatia shilingi 250,000. 

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Alchelaus Mutalemwa (pichani)amesema kijana huyo amekamatwa Oktoba 9,2018 majira ya saa moja usiku katika nyumba ya kulala wageni ‘Guest ya Five Star' Mjini Shinyanga. 

“Tulimkamata Richard Elieza Malisela ambaye ni mkazi wa Mbagala Dar es salaam kwa kufanya utapeli wa shilingi 250,000 kutoka kwa Azael Mkombolwe (30) mkazi wa Dar es salaam kwa kujifanya Afisa Usalama wa taifa kutoka Ikulu kwa lengo la kumsaidia ili amtoe ndugu wa mlalamikaji ambaye yupo gerezani kwa kosa la kupatikana na bangi”,alisema Kamanda Mutalemwa. 

Alisema mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi na atafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria. 

Na Kadama Malunde – Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post