Picha : MBUNGE AZZA HILAL AKUTANA NA VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI KATA YA USULE...AWAPIGA TAFU

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad amekutana na vikundi vya wajasiriamali katika kata ya Usule halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kuzungumza nao kisha kuwapatia michango mbalimbali ikiwemo fedha,mbegu za vitunguu,viti na majola ya batiki vyote vikiwa na thamani ya shilingi 600,000/=.

Pamoja na kusaidia vikundi hivyo vya Ujasiriamali,Mheshimiwa Azza pia aliahidi kuchangia mabati 20 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo katika shule za msingi Masunula na Usule ambavyo vinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa matundu ya vyoo.

Akizungumza na wanachama wa vikundi zaidi ya 10 katika mkutano uliofanyika leo Jumatatu Oktoba 15,2018 katika kijiji cha Igalamya,Mheshimiwa Azza Hilal aliwapongeza wananchi hao kwa kuunda vikundi vya ujasiriamali kwa ajili ya kujiinua kimaisha.

“Nimeambiwa katika kata hii kuna vikundi 35 vya wajasiriamali,kati ya hivyo 25 vimesajiliwa,na vikundi vilivyopo kwenye mkutano huu ni 13,vinajihusisha na masuala ya kilimo,ufugaji,utengenezaji sabuni na kadhalika,niwapongeze sana kwa kuchukua hatua hii,fanyeni kazi na ombeni mikopo kwenye halmashauri ya wilaya ili kukuza mitaji yenu”,alisema Azza.

Hata hivyo aliwatahadhalisha kuacha tabia ya kugawana fedha wanazopata katika vikundi vyao na badala yake wafanye kazi kwa bidii ili kukuza mitaji yao.

“Tufanyeni kazi,tuwe na vikundi vya kudumu,tusiwe na vikundi vya kugawana tu fedha,msitumie fedha zote,bakizeni ili muendelee na muweze kuwa mitaji mikubwa”,alisisitiza Azza.

“Ili kuwaunga mkono kikundi cha Batiki nakipatia jola tatu za batiki,viti vitano kwa kikundi cha ushirika,vikundi vya kilimo cha bustani navipatia makopo mawili kila kimoja,vikundi vya hisa shilingi 40,000 kila kimoja vyote vina thamani ya takribani shilingi 600,000/= na nitakuja kukagua mnaendeleaje”,alisema Azza.

“Nivishauri vikundi vya Hisa kuunda SACCOS ili viweze kupata mikopo kwenye halmashauri kwani serikali haitoi mikopo kwenye vikundi vya hisa”,aliongeza Azza.

Aidha aliwataka vijana kuunda vikundi vya ujasiriamali na kuachana na tabia ya kushinda vijiweni na wengine kuzurura ovyo huku akisisitiza kuwa mikopo inayotolewa katika halmashauri za wilaya haina riba hivyo wajitokeze kuomba ili kujiinua kiuchumi.

Katika hatua nyingine aliwataka wananchi kujitolea katika shughuli za maendeleo badala ya kusubiri serikali iwafanyie kila kitu huku akihamasisha familia kujenga vyoo ili kukabiliana na magonjwa akitumia kampeni yake ya “Afya Yangu,Mtaji Wangu”.

Awali akisoma risala ya vikundi hivyo, Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Usule Novatus Amian alisema miongoni mwa changamoto zilizopo ni ukosefu wa mikopo,ukosefu wa elimu ya ujasiriamali na usafiri kwa maafisa maendeleo ya jamii kuvifikia vikundi hivyo.

Nimekuwekea hapa chini picha za matukio mbalimbali yaliyojiri wakati wa ziara ya Mheshimiwa Azza Hilal katika kata ya Usule.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga ,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akipokelewa na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Usule Michael Mwinamila leo Jumatatu Oktoba 15,2018 katika kijiji cha Igalamya - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga ,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akivalishwa vitenge alipowasili katika kijiji cha Igalamya kwa ajili ya kukutana na wajasiriamali waliopo katika kata ya Usule halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (Vijijini).
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga ,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akipokelewa na wakazi wa kata ya Usule.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM)akiangalia sabuni ya maji iliyotengenezwa na kikundi cha Wanawake na Maendeleo kijiji cha Isholo kata ya Usule ambacho hujihusisha na utengenezaji wa sabuni za maji na mche.
Katibu wa Kikundi cha Wanawake na Maendeleo cha kijiji cha Ishololo,Joyce Charles akieleza shughuli wanazofanya kwa Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM).
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akiangalia sabuni zilizotengenezwa na Wajasiriamali kutoka kijiji cha Ishololo.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akisalimiana na Angelina Nkwabi ambaye ni Katibu wa kikundi cha Tunaweza kinachojihusisha na utengenezaji wa batiki,kilimo cha bustani.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza na wajasiriamali wa kikundi cha Ujamaa kinachojihusisha na ufugaji wa kuku wa kienyeji na kilimo cha bustani.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akisalimiana na  wajasiriamali wa kikundi cha Upendo kinachojihusisha na kilimo cha mpunga na pamba.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza na wajasiriamali wa kata ya Usule na kuwataka kuomba mikopo kwenye halmashauri ili kujiiunua kiuchumi.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza na wajasiriamali wa kata ya Usule.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga  Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akiwataka wanachama wa vikundi vya ujasiriamali kuepuka tabia ya kugawana fedha wanazopata.
Wakazi wa kata ya Usule wakimsikiliza Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akizungumza na wajasiriamali wa kata ya Usule.
Mmoja wa wakazi wa kata ya Usule akimuomba Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad aishawishi serikali kuruhusu Wazee waunde vikundi vya ujasiriamali ili wapate mikopo.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi shilingi 40,000 kwa viongozi wa kila kikundi cha Hisa ambapo alitoa shilingi 320,000 kwa vikundi vilivyokuwepo kwenye mkutano huo.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiendelea kukabidhi fedha kwa vikundi vya hisa ikiwa ni sehemu ya mchango wake kuimarisha vikundi hivyo.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi makopo ya mbegu za vitunguu kwa vikundi mbalimbali vya wajasiriamali wanaojihusisha na kilimo cha mbogamboga.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiendelea kugawa mbegu za vitunguu.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi makopo ya mbegu za vitunguu kwa wakulima wa bustani.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiwa ameshikilia jola za batiki kabla ya kukabidhi kwa kikundi cha Tunaweza kilichopo katika kijiji cha Ishololo kata ya Usule.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi jola za batiki kwa kiongozi wa kikundi cha Tunaweza.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi jola za batiki kwa kikundi cha Tunaweza.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi viti kwa kikundi cha Ushirika ambacho kinajihusisha na shughuli ya kuazimisha viti.Mheshimiwa Azza amechangia viti vitano,viti vingine ni mchango wa madiwani na wadau mbalimbali.
Wakazi wa kata ya Usule wakifuatilia matukio yalikuwa yanaendelea.
Wakazi wa kata ya Usule wakiwa katika eneo la mkutano.
Wajasiriamali wakitoa burudani ya wimbo.
Wakazi wa Usule wakiwa eneo la tukio.
Wajasiriamali wakitoa burudani ya igizo.
Igizo linaendelea.
Afisa Mtendaji wa kata ya Usule Erica Kisanga akimkaribisha diwani wa kata ya Usule akizungumza wakati wa mkutano wa Mbunge Azza Hilal katika kijiji cha Igalamya.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Usule Michael Mwinamila akizungumza wakati wa mkutano huo.
Afisa Masoko wa Benki ya NMB Tinde Thadei Mhengilalo akielezea huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa wajasiriamali.
Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Usule Novatus Amian akisoma risala ya wajasiriamali kata ya Usule.
Diwani wa kata ya Usule,Mheshimiwa Amina Bundala akielezea changamoto zilizopo katika kata ya Usule ikiwemo upungufu wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Masunula na Usule.
Diwani wa Viti Maalum Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini,Mengi Charles akiwasalimia wakazi wa kata ya Usule.
Mkazi wa kata ya Usule akiteta jambo na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad alipokutana na wajasiriamali wa kata ya Usule kwenye mkutano uliofanyika katika kijiji cha Igalamya.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post