YANGA YAICHAPA STAND UNITED 4 -3


Wachezaji wa Yanga kutoka kushoto ni Kaseke, Tshishimbi na Ngassa.

Klabu ya soka ya Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Stand United, hivyo kulinda rekodi na heshima yake dhidi ya timu hiyo kutoka Shinyanga na sasa wamefikisha mechi 8 za kushinda kati ya 9 walizokutana.

Katika mchezo wa leo mabao ya Yanga yamefungwa na Mrisho Ngassa dakika ya kwanza, Ibrahim Ajibu dakika ya 32, Andrew Vicent dakika ya 35 na Deus Kaseke dakika ya 57.

Kwa upande wa Stand United mabao yao yote yamefungwa na Alex Kitenge ambaye amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu kwenye mechi moja 'Hat-trick' ya ligi kuu msimu huu. 

Pamoja na ushindi wa Yanga leo, lakini mlinda mlango mpya wa Yanga Klaus Kindoki raia wa DR Congo, hatakuwa na furaha kutokana na makosa kadhaa aliyoyafanya hususani kwenye bao la kwanza na la pili ya Stand United. Kindoki alikuwa anacheza mechi yake ya kwanza tangu asajiliwe na Yanga.

Stand United sasa imeshinda mechi mbili kwenye mechi zake 4 za kwanza msimu huu, huku Yanga wao wakishinda mechi yao ya pili msimu huu hivyo kufikisha alama 6.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post