WATU WANNE WAFARIKI KATIKA AJALI YA GARI LA KUBEBA MBAO ROMBO


Na Dixon Busagaga,Rombo.

WATU wanne wakiwemo wawili wa familia moja wamefariki dunia papo hapo baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Isuzu kuacha njia na kwenda kugonga ngema katika eneo la Kikelelwa wilayani Hai.

Waliofariki dunia wametambulika kwa majina ya Emanual Josephat Silayo (28) ,Viviano silayo (35) wakazi wa Mbomai Juu,Juma Idd (20) maarufu kama mwarabu na mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Deolla.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Hamis Issah aliyefika eneo la tukio amethibitisha kutokea kwa ajalo hiyo na kwamba dereva wa Lolri hilo lililokuwa limebeba mbao alikimbia kusiko julikana baada ya ajali.

"Jitihada za kumtafuta dereva zinafanyika na chanzo cha ajali ni kupoteza muelekeo kwa Lori hilo na baadae kugonga Gema ndipo watu waliokuwa wanekaa mbele walichomoka na kwenda kupigiza vichwa katika Gema na kupasuka"alisema Kamanda Issah.
Kamanda Issah amesema gari hilo likiwa na shehena ya mbao lilikuwa likitokea eneo la West Kilimanjaro ,eneo maarufu kwa uchanaji wa mbao na kwamba lilikiwa likielekea Rombo kupitia njia ya Rongai.

"Ni gari la kubeba mbao lilikua linatoka West Kilimanjaro kupitia njia ya Kikelelwa wilayani Rombo ,Gari aina ya Isuzu likiwa na namba za usajili T 889 ACN lilimshinda dereva na kuacha njia na baadae kugonga ngema iliyosababisha watu wanne waliokuwemo katika gari hilo kufa papo hapo." alisema Kamanda Issah.

Miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika hosptali ya wilaya ya Rombo kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah akiangalia gari hilo wakati alipofika kwenye eneo la tukio.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post