VIFO AJALI MV NYERERE YAFIKIA 136..UTAMBUZI WA MIILI UNAENDELEA.....RAIS KENYATTA, KAGAME WATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI


Hadi sasa ni watu 136 wamethibitishwa kufa kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere nchini Tanzania huku makundi ya uokoaji yakirejelea shughuli za kuwatafuta manusura.

Afisa mkuu wa Polisi Tanzania Simon Sirro anasema kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na mkasa huo imefikia 136, shirika la habari la Reuters linaripoti.

Inahofiwa wengine wengi bado hawajulikani waliko na kwamba huenda watu 200 wamezama. 

Akizungumza katika kituo cha Afya Bwisya leo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Issack Kamwelwe amesema miili 36 tayari imetambuliwa na ndugu na jamaa wakati kazi ya kuitambua iliyosalia ikiendelea. 

Kivuko cha MV Nyerere kilichozama jana mchana Septemba 20, 2018.

Kenyatta na Kagame watuma salamu za rambirambi

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametuma salamu za rambirambi kwa Rais Magufuli na Watanzania kwa jumla kutokana na mkasa huo. Amesema Wakenya wako pamoja na "ndugu zao" Watanzania kipindi hiki kigumu.On behalf of the people of Kenya and on my own behalf, I express our most sincere condolences to my brother President @MagufuliJP and our dear neighbour of the United Republic of Tanzania🇹🇿 following the tragic capsizing of MV Nyerere in the Lake Victoria Waters.I express our solidarity and support with our brothers and sisters in Tanzania🇹🇿, with whom we've been friends and have deep ties, and to assure them that we will lend every needed support.Rais wa Rwanda Paul Kagame pia ametuma salamu za rambirambi kwa jamaa na wapendwa wa waathiriwa wa mkasa huo wa kuzama kwa kivuko Mwanza.Our deepest condolences to the families and loved ones of the victims of the Lake Victoria ferry accident. Our thoughts are with you. We cannot thank the rescuers enough.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post