Friday, September 7, 2018

TUNDU LISSU : NIMEWA - MISS WATANZANIA...NITARUDI

  Malunde       Friday, September 7, 2018

“Nimei-miss sana Tanzania na nimewa-miss Watanzania.” Hii ndiyo kauli ya Tundu Lissu leo Septemba 7 anapotimiza mwaka mmoja tangu ashambuliwe kwa risasi mjini Dodoma.

Lissu, ambaye hadi sasa amefanyiwa upasuaji mara 21 katika mwili wake, amefanya mazungumzo maalumu na Mwananchi na kueleza masuala mbalimbali huku akisisitiza, “Nitarudi.”


"Mwaka mmoja umekuwa mrefu na mgumu sana kwangu sio kwa sababu ya majeraha ya mwili. Ni kwamba pia nimei-miss sana Tanzania na nimewa-miss Watanzania. 

Nime-miss sana Bunge, licha ya matatizo yote ya Bunge la Spika Ndugai. Nimewa-miss sana watu wangu wa Jimbo la Singida Mashariki na mikutano yetu ya hadhara. 

Nime-miss sana kazi zangu za chama na nimewa-miss viongozi wenzangu, wanachama wetu na wafuasi wetu katika mamilioni yao. 

Nime-miss sana mapambano ya utetezi wa haki za watu wetu ndani na nje ya Mahakama. 

Nimewa-miss mawakili wa Tanzania Bara walionipa heshima ya kuwaongoza katika kipindi kigumu sana katika historia ya TLS. 

Mshairi Sipho Sepamla aliandika shairi lingine liitwalo 'The Exile', yaani 'Uhamishoni.' Shairi hilo linaelezea machungu ya kuishi uhamishoni kwa kulazimishwa wakati wa utawala wa kibaguzi wa makaburu wa Afrika Kusini.

Katika huu mwaka mmoja wa kulazimishwa kuwa nje ya nchi; wa kutokuonana moja kwa moja na watu wetu, familia, ndugu, jamaa, majirani na marafiki zangu; wa kufuatilia mapambano ya kudai haki na demokrasia mitandaoni badala ya kuwa mshiriki kwenye uwanja wa mapambano, sasa ninaelewa maana hasa ya kuwa 'uhamishoni.'

 Baada ya kushindwa na Wajapan kwenye Mapigano ya Bataan nchini Ufilipino mwaka 1942 wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, kamanda wa majeshi ya Marekani katika Bahari ya Pacific ya Magharibi, Jenerali Douglas MacArthur, alitamka: 'I Shall Return.' 'Nitarudi.' 

Na mimi nawatamkia Watanzania: 'Nitarudi!!!'"

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post