Saturday, September 29, 2018

RAIS MAGUFULI ATOA ONYO KWA MABALOZI WANAOKWENDA NJE 'KUNYWA WINE'

  Malunde       Saturday, September 29, 2018
Rais John Magufuli, amewataka mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje, kufanya kazi waliyotumwa au wajiandae.

Akizungumza baada ya kumwapisha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro aliyemteua wiki hii baada ya kutengua uteuzi wa Dk. Susan Kolimba, amesema hatamvumilia balozi asiyefanya kazi.

“Kama kuna balozi atakwenda kule kunywa ‘wine’ miezi sita yote bila kufanya kazi ajiandae… wizara hii ina mambo ya ajabu sana Balozi wetu kule China, ameandika barua zaidi ya 24 zilizojibiwa ni mbili ndiyo maana nikaamua kutoa Naibu Waziri na Katibu Mkuu wake,” amesema.

Kwa upande wake Dk. Ndumbaro amesema atakwenda kutekeleza kufanya kazi kwa mujibu wa maelekezo aliyopewa.

“Nikuahidi rais nitakwenda kutekeleza maagizo hayo kwa mujibu wa maelekezo uliyotoa, nitatekeleza majukumu ya Katiba na kufuata Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ukurasa 110 hadi 111 inayoongelea masuala ya kimataifa,” amesema Dk. Ndumbaro.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post