PROF MDOE:TANZANIA IKO TAYARI KUSHIRIKIANA NA IAEA KATIKA KUENDELEZA MATUMIZI SALAMA YA NGUVU ZA NYUKLIA


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe ameongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano Mkuu wa 62 wa kimataifa wa kuendeleza matumizi salama ya nguvu za nyuklia unaofanyika mjini Vienna nchini Austria.

Akizungumza katika mkutano huo mjini Vienna Profesa Mdoe ameishukuru IAEA kwa kuisaidia nchi ya Tanzania mashine ya kuchunguza na kutibu saratani ambayo inatumika katika hospitali ya Bugando iliyopo mkoani Mwanza na misaada ya kiufundi katika hospitali ya Saratani ya Ocean Road iliyopo jijini Dar es salama pamoja na misaada ya kuwasomesha wataalam kwenye eneo la Teknolojia ya nguvu za nyuklia.

Profesa Mdoe pia amekieleza kikao hicho Cha kimataifa kuwa nchi ya Tanzania iko tayari kushirikiana na IAEA katika kuendeleza matumizi salama ya nguvu ya nyuklia.

Balozi wa kudumu kwenye Mashirika ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva nchini Uswis James Msekele naye anashiriki mkutano huo.

Mkutano huo ulioanza Septemba 17 utahitimishwa Septemba 21, 2018 huko mjini Vienna nchini Austria.

Imetolewa na:

Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
19/9/2018

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527