ORODHA YA VYUO VILIVYOFUTIWAA UDAHILI KWA WANAFUNZI NA TCU, VILIVYOFUTWA

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), imesitisha masomo na udahili wa wanafunzi wapya kwa ngazi zote za masomo na katika programu kwenye baadhi ya vyuo vikuu kutokana na kukosa vigezo.

Pia imefuta vituo viwili vya vyuo vikuu na kuamuru wanafunzi wanaoendelea na masomo wahamishwe.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumanne Septemba 25, Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa amevitaja vyuo hivyo kuwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala nchini (KIUT), Chuo cha Teofilo Kisanji (TEKU), Chuo Kikuu kishiriki cha Marian (MARUco) na Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Kardinali Rugambwa (CARUMUCo).

Vyuo vingine ni Chuo cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU), Chuo kikuu cha Mt. Yohana cha Tanzania (SJUT-St. Marks Centers na Chuo kikuu cha Umoja wa Afrika Tanzania (UAUT).


Vyuo hivyo ni pamoja na Chuo kikuu Teofilo Kisanji, Kituo cha Tabora na Chuo kikuu Mt. Yohana cha Tanzania, Msalato (SJUT -Msalato Center).


Aidha, amevitaja vyuo vilivyositishiwa utoaji mafunzo na kuamuru wanafunzi wote wanaoendelea na masomo wahamishwe kuwa ni Mlima Meru (MMU), Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UoB), Chuo cha Eckernforde Tanga (ETU) cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta Kituo cha Arusha na Chuo Kikuu Kishiriki cha Josiah kibira (JOKUCo).


“Asitokee mwanafunzi yeyote akasajiliwa katika vyuo hivyo na wanaotakiwa kuhama wawasiliane na vyuo vyao haraka,” amesema Profesa Kihampa.


Kwa upande wake mwakilishi kutoka Bodi ya Mikopo (HELSB), Deus Changala amesema waliokuwa na mikopo wasiwe na wasiwasi itapelekwa watakapokuwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527