Picha : BENKI YA NMB MANONGA YAADHIMISHA SIKU YA USAFI DUNIANI KWA KUFANYA USAFI SOKO KUU MJINI SHINYANGA


Benki ya NMB Tawi la Manonga mkoani Shinyanga imeadhimisha siku ya Usafi Duniani kwa kusafisha mazingira katika soko kuu la mjini Shinyanga ili kuunga juhudi za serikali za utunzaji wa mazingira.


Leo ni siku ya usafi duniani ambapo huadhimishwa kila Septemba 15, ambapo wafanyakazi wa Benki hiyo wakiongozwa na Meneja wao Baraka Ladislaus wameamua kuadhimisha siku hiyo kwa kufanya usafi wa mazingira katika soko kuu la mjini Shinyanga.

Akizungumza mara baada ya kumaliza kufanya usafi kwenye soko hilo Meneja wa Benki ya NMB Manonga Baraka Ladislaus amesema wao ni sehemu ya jamii hivyo wameamua kujitoa kushiriki zoezi la usafi wa mazingira na wataendelea kushiriki mara kwa mara katika maeneo mengine ili kuunga juhudi za Serikali za utunzaji wa mazingira.

“Sisi ni sehemu ya jamii ambapo tumeamua leo kabla ya kwenda kazini tuanze kwanza na shughuli za usafi wa mazingira katika soko kuu la mjini Shinyanga kama sehemu ya kuadhimisha siku ya usafi duniani, na zoezi hili litakuwa endelevu kwa kushiriki siku ya usafi wa mazingira kila jumamosi ya mwisho wa mwezi katika maeneo mengine,”amesema Ladislaus.

“Na katika soko hili tumebaini kuwepo na changamoto ya uhaba wa vifaa vya usafi wa mazingira, ambapo sisi kama Benki ya NMB tutajipanga siku si nyingi tutawapelekea vifaa hivyo,”ameongeza.

Naye mwenyekiti wa Soko hilo Alex Steven ameipongeza Benki hiyo ya NMB kwa kushiriki zoezi la usafi wa mazingira, huku akitoa wito kwa wafanyabiashara kuendelea kuwa na juhudi za utunzaji wa mazingira ,ili kujikinga na magojwa ya mlipuko yasiweze kutokea kikiwamo kipindupindu.


TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA


Meneja wa benki ya NMB Tawila la Manonga mkoani Shinyanga Baraka Ladislaus akizungumza baada ya kumaliza zoezi la usafi wa mazingira katika Soko kuu la mjini Shinyanga na kuahidi kuendelea kuunga juhudi za serikali za utunzaji wa mazingira.Picha zote na Marco Maduhu -Malunde1 Blog

Mwenyekiti wa soko kuu la mjini Shinyanga Alex Steven akiipongeza Benki hiyo ya NMB kufanya usafi wa mazingira katika soko hilo na kulifanya kuwa katika hali ya usafi.

Wafanyakazi wa Benki ya MNB Manonga mkoani Shinyanga wakifanya usafi wa mazingira katika eneo la Soko kuu mjini Shinyanga.

Kulia ni Mwenyekiti wa soko kuu Alex Steven akiwa na mfanyakazi wa benki ya NMB Manonga mkoani Shinyanga wakifanya usafi wa mazingira katika soko hilo.

Usafi ukiendelea katika soko kuu la mjini Shinyanga.

Meneja wa Benki ya NMB Manonga mkoani Shinyanga Baraka Ladislaus akifagia uchafu katika soko kuu la mjini Shinyanga.

Wafanyakazi wa benki ya NMB Manonga wakizoa uchafu katika soko kuu la mjini Shinyanga.

Usafi ukiendelea.

Meneja wa benki ya NMB Manonga mkoani Shinyanga Baraka Ladislaus akizungumza kwenye zoezi hilo la usafi wa mazingira katika soku kuu la mjini Shinyanga na kubainisha kuwa wakimaliza usafi huo watarejea kazini kwenda kuhudumia wananchi.

Meneja wa benki ya NMB Manonga mkoani Shinyanga Baraka Ladislaus akiendela na usafi wa mazingira katika soko kuu mjini Shinyanga.

Usafi ukiendelea.

Wafanyakazi wa Benki ya NMB wakiendelea na usafi.

Usafi ukiendelea.Usafi ukiendelea katika maeneo mbalimbali ya soko hilo.

Wafanyakazi wa benki ya NMB Manonga wakipiga picha ya pamoja na mwenyekiti wa soko kuu la mjini Shinyanga Alex Steven wa kwanza mkono wa kushoto ,mara baada ya kumaliza kufanya usafi wa mazingira katika soko hilo.

Picha zote na Marco Maduhu -Malunde1 Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post