MKURUGENZI WA TUME YA UCHAGUZI AMPA SIKU SABA MBOWE AOMBE RADHI


Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dr Athumani Kihamia ametoa siku saba kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe kumuomba radhi kwa kile alichokidai kiongozi huyo kutoa maneno yaliyoashiria kumkashifu.

Kwa mujibu Dkt. Kihamia kwenye mkutano wa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na Waandishi wa habari alitamka kuwa mkurugenzi Kihamia akachukue fomu ya kuwania nafasi ya Uongozi katika baadhi ya maeneo ya Uchaguzi kwa madai kiongozi huyo anatumika na Chama Cha Mapinduzi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Dkt. Athumani Kihamia amesema "Mbowe anatakiwa achague maneno ya kusema, kwa upande wa CHADEMA yeye ni kiongozi mkubwa, ninataka aniombe radhi ndani ya siku 7 na nimeshaongea na wasaidizi wake akina Mrema na John Mnyika wamwambie kiongozi wao aniombe radhi.."

Kuhusiana na hoja zilizolalamikiwa na CHADEMA na kupelekea kujitoa kushiriki kwenye uchaguzi wa marudio utakaofanyika katika jimbo la Liwale na baadhi ya kata Dr Kihamia amesema, "tume haina mpango wa kuongeza vituo hewa wala kupunguza vituo isipokuwa tunatumia vituo vilevile vya 2015 mpaka tutakapohakiki tena orodha ya daftari la kudumu la wapiga kura."

Jana Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kilitangaza kujiondoa rasmi kushiriki chaguzi ndogo zote zilizotangazwa kufanyika hivi karibuni na chaguzi zozote zitakazofuata zinazosimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa madai kwamba tume hiyo inafanya kazi ya Chama Cha Mapinduzi.

Chanzo-EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527