WALIOFARIKI KWENYE KIVUKO CHA MV NYERERE WAFIKIA 224


Idadi ya miili ya watu iliyoopolewa katika ajali ya kivuko cha Mv Nyerere imefikia 224 baada ya miili mingine kupatikana leo Septemba 23, 2018.

Akizungumza leo asubuhi Septemba 23,2018 Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema wanaendelea kutoa taarifa zaidi za upatikanaji miili hiyo kadiri inavyopatikana na kwamba baadhi ya maiti zilizokuwa zimezama chini ya maji, zimeanza kuibuka na kuelea na tangu alfajiri miili minne imeonekana na kuopolewa katika fukwe za Bwisya.

Mongella  uchimbaji wa makuburi unaendelea kwa ajili ya maziko ya miili ambayo haijatambuliwa.

Makaburi hayo yanachimbwa hatua zaidi ya 250 kutoka gati la Bwisya ambako shughuli za uokoaji zinaendelea.

Mongella amesema wapo marehemu waliotambuliwa na ndugu zao lakini wakaomba wazikwe katika utaratibu ulioandaliwa na Serikali.

Via MWANANCHI


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post