MGOMBEA URAIS BRAZIL ACHOMWA KISU KWENYE MKUTANO WA KAMPENI

Mgombea Jair Bolsonaro alibebwa na wafuasi wake baada ya kuchomwa na kisu

Mgombea anayeongoza anaeminika anaweza kushinda uchaguzi nchini Brazili Jair Bolsonaro, amechomwa kisu wakati wa kampeni zake , mgombea huyo wa mrengo wa kulia alichomwa kisu katika mkutano mkubwa wenye mkusanyiko wa watu wengi katika eneo la kusini mashariki.

Mwanasiasa huyo ambaye amekua gumzo kwa maoni yake juu ya ubaguzi wa rangi , amepata kura nyingi katika kura za maoni za hivi karibuni.

Kura hizo za maoni zinaonesha kuwa anatafanya vizuri katika uchaguzi wa urais mwezi ujao na kumpita Mgombea na Rais wa zamani Lula da Silva.

Tukio hilo lilitokea vipi?

Picha za video zimemuonesha bwana Bolsonaro akinyoosha mkono kwa wafuasi wake na hapo ndipo alipochomwa na kitu ambacho baadae iligundulika na kisu

Baada ya hapo aliinama kwa maumivu na haraka wafuasi wake walimshusha chini na kumuingiza ndani ya Gari kisha kupelekwa Hospitali.

Baada ya shambulio hilo, mtoto wake aliandika katika mtandao wa Twitter kuhusu taarifa hiyo lakini baadae masaa mawili mbele alitoa maelezo kwa kina.

''kwa bahati mbaya amekua na hali mbaya kuliko tulivyodhani, amepoteza damu nyingi amefika hospitali na damu 10/3 karibu afariki, lakini sasa anaendelea vizuri tafadhali tumuombee'' aliandika katika mtandao wa Twitter.

Wauguzi wa hospitali baadae walisema kuwa bwana Bolsonaro amepata jeraha kubwa na limechimba sana kwenye utumbo lakini sasa anaendelea vizuri.

Alipelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa muda wa masaa baada ya upasuaji, lakini atasalia hospitali hadi siku kumi.

Polisi wanasema kuwa wamekamata mshukiwa wa tukio hilo anaitwa Adelio Obispo de Oliveira .

watu mbalimbali wamekosoa vikali mshukiwa huyo kwa kitendo alichokifanya.
Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post