MBOWE: NILIWEKWA NA WANACHAMA...SIONDOKI UENYEKITI CHADEMA KWA KELELE ZA WATU

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema kamwe hatoachia kiti hicho kwa kusikiliza maneno ya watu wa nje ya chama ambao hata hawakumchagua.

Mbowe amesema hayo leo Septemba 19, 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Chadema, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Amesema chama hicho kufanya vibaya sababu si yeye, “Na mimi niliwekwa na wanachama, wakitaka wataniondoa lakini siondoki kwa kelele za watu.”

Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni amesema kamwe hatakuja kukipigia magoti chama tawala cha CCM.

Amesema hata siku moja CCM haitafurahi kumuona anakuwa na nguvu kwenye chama, lengo lao ni kuona anakuwa dhaifu.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.