MAAGIZO YA RC GAMBO KATIKA ZIARA YAKE HALMASHAURI YA MERU


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Maashaka Gambo akisisitiza ukusanyaji wa mapato kwa ngazi ya Halmashauri kwa Serikali Kuu.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akitoa taarifa ya usimamizi wa Shughuli za Serikali wakati wa Ziara ya MKuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo. 
Mwenye kiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Will Njau akisalimia wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa kwenye Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Emmanuel Mkongo akisoma taarifa ya Halmashauri hiyo wakati wa kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na vitengo Halmashauri ya Meru wakati wa kikao cha Mkuu wa Mkoa na watumishi wa Halmashauri hiyo.
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo.
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo.
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo. 
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo.
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo. { Picha zote na Imma Msumba }

Na Flora Joseph , Arumeru

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameziagiza Halmashauri zote za Mkoa huo kusimamia vyema swala la ukusanyaji wa Mapato sambamba na kuipa ushirikiano wa kutosha Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA).

Mhe.Gambo ametoa agizo hilo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru katika ziara yake ya kukagua shughuli za maendeleo haswa miradi ya Afya.

Mhe.Gambo amesema taarifa ya Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa mwaka wa fedha 2018/2019 iliyotelewa inaonesha makisio ya makunyanyo ya mapato ya ndani ni bilioni 4 huku bajeti ya mishaara ya watumishi inayotoka serikali kuu ni bilioni 39,hivyo amesisitiza Halmashauri kukusanya mapato ya ndani na kuipa ushirikiano Serikali kuu katika ukusanyaji wa mapato kwani kwa Kiasi kikubwa bajeti za Halmashauri zinaitegemea Serikali kuu "toeni ushirikiano kwa TRA iweze kukusanya mapato ya kutosha kwa Serikali kutoa huduma bora za Afya,Elimu na Maji kwa wananchi wake sambamba na kuwalipa watumishi mishaara" amesisitiza Gambo.

Mhe.Gambo ameongeza kuwa mapato ya ndani ya Halmashauri lazima yatumike kuwalete wananchi maendeleo ambapo ,ameelekeza utoaji wa asilimia 10 za mapato kwa ajili ya mfuko wa wanawake,vijana na walemavu kutolewa kwa wakati sambamba na asilimia 60 za mapato ya Halmashauri kutumika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Mhe.Gambo amemwagiza Mkurugezi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Emmanuel Mkongo kuhakikisha fedha kiasi cha milioni 55 za mfuko wa wanawake vijana na walemavu ambazo hazikutolewa kwa mwaka wa fedha ulioisha 2017/2018 kutolewa .

Aidha ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru ni muendelezo wa Ziara yake Mkoani humo inayolenga kukagua shughuli za maendeleo aswa utekelezaji wa miradi ya Afya,ziara hiyo ilianza katka Halmashauri ya Mji wa Arusha na kufuata Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Ambapo leo inatarajiwa kuhitimika katika Halmashauri hii ya Wilaya ya Meru

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post