MAADHIMISHO YA SIKU YA WAZEE KITAIFA KUFANYIKA ARUSHA , RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI MZEE ALHAJI ALLY HASSAN MWINYI KUWA MGENI RASMI


Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Alhaji Ally Hassan Mwinyi


Na. VERO IGNATUS, ARUSHA

Wakati tukielekea kusherehekea siku ya wazee Septemba 30 imeelezwa kuwa zaidi ya asilimia 80% (takriban milioni 2) ya wazee hapa nchini wanaishi vijijini. 

Akizungumza na vyombo vya habari kamishna wa ustawi wa jamii kutoka wizara ya Afya jinsia wazee na watoto Dkt. Naftali Ng’ondi amesema kuwa juhudi za ziada zinashitajika ili kuwafikia na kuweza kuhakikisha wanapata huduma stahiki kama ilivyo katika sera ya Taifa. 

Ng'ondi amesema maadhimisho ya siku ya wazee duniani kitaifa yatafanyika jijini Arusha ambapo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais mstaafu wa awamu ya pili Mzee Alhaji Ally Hassan Mwinyi


Aidha kwa mujibu wa shirika la Help Age International limeweka wazi kuwa hapa nchini asilimia 27% ya wazee wote (677,043) wanaishi wenyewe bila msaada wa mtu yeyote.

Amesema kuwa zaidi ya asilimia 83% ya wazee wote (2.1m) wanaishi katika familia na kupata angalau matunzo ya familia tofauti na wenzao ambao wanaisha wangali pekee yao.

Nchini Tanzania kuna familia ambazo wazee wamekuwa wakibeba majukumu ya kuwalea watoto yatima kama takwimu zinavyoonyesha asilimia 40% ya watoto yatima wanalelewa na familia za wazee.

Mara baada ya uzinduzi wake kesho wazee watapata fursa ya kupata huduma ya kupima afya kupata ushauri wa kitabibu pamoja na ufunguzi wa maonyesho ya kazi mbali mbali za mikono zinazofanywa na wazee.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Wazee ni Hazina ya Taifa: Tuenzi Juhudi za Kutetea Haki na Ustawi Wao’’. Kaulimbiu hii inahimiza Serikali na Jamii kwa ujumla kutambua na kuenzi jitihada za Wazee katika ujenzi wa Taifa letu.

“Tarehe moja mwezi ujao itakuwa siku ya wazee nawaombeni nyote kujitokeza kwa wingi wakiwemo wazee wetu kwenye uwanja wa sheikh Amri Abeid”,alisema Dkt.Ng’ondi

Mmoja ya wazee aliohojiwa mkazi wa jiji la Arusha Swalehe Allly amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano inatakiwa kuonyesha juhudi zake kwa kuwaandalia wazee wetu angalau pensheni kama takwimu zinavyoonyesha kuwa Tanzania Bara 96% ya wazee wote hawana pension ya uzeeni

Amesema kuwa tuige mfano na kuonyesha juhudi za serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa kuwapatia Wazee 58,371 kati yao 27,000,(46 %) wanapata pensheni wenye umri wa Miaka 70


“Hapa utaona jinsi maisha ya uzee yalivyo kuwa na mtihani kama juhudi za maksudi hazitachukuliwa na serikali zetu kote ulimwenguni kuhakikisha wazee wanapata matunzo stahiki kama tawimu hizi” ,alisema Ally

Imeonyesha juhudi kama hazitachukuliwa na kufanyiwa kazi, asilimia Zaidi ya 50% ya familia za wazee wanaishi chini ya kiwango cha umaskini. kigezo- Benki ya Dunia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527