AJALI YAUA WATALII WANNE ARUSHA


Na Mussa Juma, Mwananchi 

Monduli. Watu watano wamefariki dunia wakiwamo watalii wanne kutoka nchi za Hispania na Italia baada ya gari la utalii kugongana na lori katika eneo la Nanja, wilayani Monduli mkoani Arusha.

Mkuu wa wilaya ya Monduli, Idd Kimanta, akizungumza na Mwananchi leo Jumapili Septemba 2, 2018 amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema waliofariki ni watalii wanne, ambao uraia wao ni wa nchi za Hispania na Italia ambapo mwingine aliyefariki ni mpishi wa watalii hao.

"Nipo eneo la tukio tayari tumepeleka miili Hospitali ya Mount Meru na hadi sasa hali ya dereva wa gari la utalii si nzuri." amesema.

Amesema gari lililopata ajali ni la kampuni ya Tabia Tours ya jijini Arusha, ambapo tayari uchunguzi wa tukio umeanza.

"Kamanda wa polisi nimemuacha eneo la tukio wanaendelea kujua nini chanzo cha ajali hii" amesema.

Kamanda wa polisi mkoa Arusha, Ramadhani Ng'azi amethitisha kutokea ajali hiyo na kueleza kuwa, atatoa taarifa za ajali hiyo mapema baada ya kupata taarifa muhimu ikiwepo uraia wa watalii, chanzo cha ajali na hali za majeruhi.
Chanzo- Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post