JULIUS KALANGA ATANGAZWA MSHINDI UCHAGUZI WA UBUNGE MONDULI

Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi wa Jimbo la Monduli, Steven Ulaya ametangaza matokeo ya Jumla ya Ubunge katika jimbo la Monduli.

Uchaguzi huo ulihusisha jumla ya vyama nane vya siasa vilivyo kuwa vinawania nafasi hiyo ya kupewa ridhaa na wananchi ya kuongoza jimbo hilo hadi mwaka 2020.

Julius Kalanga wa CCM (Pichani) ametangazwa mshindi wa kiti cha Ubunge katika Jimbo hilo baada ya kupata kura 65, 714 dhidi ya kura 3,187 alizopata mshindani wake Yonas Leiser wa CHADEMA.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post