DKT NDUGULILE ATOA MWEZI MMOJA KWA UONGOZI TAASISI YA USTAWI WA JAMII KUTATUA CHANGAMOTO ZAKE


 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akisikiliza ripoti ya utendaji kazi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Taasisi Dkt. Zena Mabeyo.
 Wajumbe wa menejimenti ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii wakimsikiliza Mh. Naibu waziri Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipokutana nao Jana.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. faustine Ndugulile akizungumza na Watumishi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii.
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile  akipokelewa na Kaimu Mkuu wa Taasisi Ya Ustawi wa Jamii  Dkt Zena Mabeyo alipofika kutembelea Taasisi hiyo jana,jijini Dar Es Salaam.
Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) amefanya ziara katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii ikiwa ni miongoni mwa ziara ya kutembelea taasisi zilizo chini ya wizara yake katika kuboresha utendaji kazi. 

Dkt Ndugulile jana Septemba 27,2018, pamoja na kufanya ziara  katika taasisi hiyo na kujionea mazingira halisi,pia alifanya mkutano na menejimenti, wafanyakazi pamoja na viongozi wa serikali ya wanafunzi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii,ambapo pamoja na mambo mengine Mh Naibu Waziri alisomewa taarifa ya maendeleo ya taasisi na mipango ya baadae. 

“Nimeskia taarifa nzuri ya maendeleo na mafanikio pamoja na changamoto za Taasisi, nawaagiza viongozi kutatua changamoto ambazo ziko ndani ya uwezo wenu na sisi kama serikali tutazifanyia kazi zile zinazotuhusu. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa huduma zinaendelea kutolewa kwa ubora na maslahi ya watumishi yanaboreshwa”. Alisema Dkt. Ndugulile. 

Aidha Ndugulile ametoa maagizo kwa menejimenti ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii kufanyia kazi kwa muda mwezi mmoja tu,baadhi ya mambo ambayo ameona yanahitaji ufumbuzi wa mapema ili kuboresha mazingira ya utoaji huduma katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii. 

Katika kuhitimisha mkutano wake na uongozi, wafanyakazi pamoja na serikali ya wanafunzi wa Taasisi, Mh. Naibu Waziri Dkt. Ndugulile amepongeza kazi nzuri inayofanywa na watumishi na ameahidi wao kama Wizara kuendelea kushirikiana na Taasisi ya Ustawi wa jamii katika kutoa huduma bora zinazokidhi mahitaji ya wananchi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527