DC PANGANI AWATAKA WASHIRIKI WA MISS TANZANIA KUTANGAZA UTALII


Washiriki wa Miss Tanzania 2018.

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Pangani Zainab Abdallah amewataka washiriki wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania mwaka 2018 kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Amesema lengo ni kusaidia kuongeza idadi ya watalii nchini huku akiwahakikishia warembo hao Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli imeamua kutoa kipaumbele kwa vijana kutimiza ndoto zao.

Abdallah ambaye ndio Mkuu wa Wilaya mwenye umri mdogo kwa wakuu wa wilaya nchini amesema hayo wilayani Muheza mkoani Tanga baada ya kuwapokea warembo 20 wanaoshiriki shindano hilo.

Ambapo walifika mkoani Tanga kwa ajili ya kutembelea vituo vya utalii vinavyosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu nchini(TFS) ambapo amewahakikishia kwenye hifadhi hiyo kuna utalii ambao haupo mahali kokote duniani zaidi ya Misitu ya Amani.

Hivyo amesema ujio wa warembo huo ni muhimu na kuwataka wawe mabalozi wazuri wa kuutangaza utalii

"Tanzania ina vivutio vingi sana,mfano kwa wilaya ya Pangani tuna mbuga Sadan ambayo ndio mbuga ambayo imepakana na bahari barani Afrika.

" Pia tuna majengo ya kale kwa kifupi Pangani haitofautiani na Zanzibar.Tujitahidi kuutangaza utalii wa ndani ili tusaidie kuleta pato la Taifa,"amefafanua.

Ameongeza kupitia utalii wa ndani warembo hao watajipambanua kwakutumka fursa zilizopo ili kujipatia fursa za ajira.

Wakati huo huo Meneja Masoko na Uwekezaji wa TFS Mariam Kobelo ameeleza kwamba malengo ya kuwapeleka warembo hao katika vivutio hivyo ili waone vivutio na kisha kuvitangaza vivutio.

"TFS itatumia warembo hao kama chombo cha kutangaza utalii wandani kwa upande wa mazingira,kwa kufanya hivyo watasaidia kuongeza pato kwa sbabu tutawatumia kama chombo cha kutangaza utalii wa mazingira,mito inayoteteresha maji,misitu na vinginevyo.

Warembo hao kwa wakiwa katika hifadhi ya msitu asili wa Amani wamepata nafasi ya kuelezwa vivutio vinavyopatikana na hasa vinyonga wa pembe tatu ambao wanapatikani katika hifadhi hiyo.

Kwa upande wa warembo hao wamefurahishwa kutembelea hifadhi hiyo kwani wamepata nafasi ya kushuhudia vivutio mbalimbali vya utalii.

Kwa kukumbusha mashindano ya Miss Tanzania yanatarajia kufanyika Septemba 8 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post