Sunday, September 2, 2018

ASKOFU ASHAMBULIWA BAADA YA KUMSHIKA TITI MSANII KWENYE IBADA

  Malunde       Sunday, September 2, 2018
Huko nchini Marekani Askofu aliyekuwa akiongoza ibada ya mazishi ya gwiji wa muziki nchini humo, Aretha Franklin amejikuta akishambuliwa mtandaoni baada ya kuonekana akishika titi la msanii Ariana Grande wakati ibada ya mazishi ikiendelea.


Picha na video zinamuonyesha Askofu Charles H Ellis wakimshika Ariana juu ya kiuno chake huku vidole vyake vikiwa vimeshikilia upande mmoja wa kifua chake.


“Sio lengo langu kumshika mwanamke matiti”, aliambia shirika la habari la AP.


Aliongeza, “Pengine nilivuka mpaka, pengine nilijihisi kuwa karibu naye sana kama rafiki. Lakini tena naomba msamaha. Muhubiri huyo balisema kuwa aliwakumbatia wasanii wote waume kwa wake wakati wa shrehe hiyo ya kumuaga malkia wa muziki wa soul.


Lakini waliohudhuria walianza kutuma picha kutoka katika ibada hiyo wakati Ariana aliposimama na kuanza kuimba wimbo wa Aretha Franklin ‘You Make Me Feel a natural Woman’


Watu wengi walihisi kwamba mkono wa Askofu Ellis ulikuwa juu zaidi ya mwili wa mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 25 alipokuwa akizungumza naye na kusema kuwa hakupendelea kushikwa hivyo
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post