AJALI MV NYERERE : MIILI ZAIDI YA 125 WALIOFARIKI YAOPOLEWA ZIWA VICTORIA

Mpaka saa Saa 7:00 Mchana, Septemba 2,2018  Miili zaidi ya 125 imepatikana zoezi la uokoaji linaendelea

Mpaka sasa miili zaidi ya 125, imepatikana katika ajali ya kivuko cha MV. Nyerere kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella na zoezi la uokoaji linaendelea

Saa 6:40 Mchana, Septemba 21: Jeshi la Polisi kufungua Jalada la uchunguzi

Mkuu wa Jeshi la Polisi, Nchini (IGP) Simon Sirro amesema kuwa litafunguliwa Jalada maalum la kuchunguza tukio la kuzama kwa kivuko cha MV. Nyerere jana, Septemba 20 mita chache kabla ya kuwasili katika kisiwa cha Ukara.

IGP Sirro amesema kuwa kwa sasa zoezi la utambuzi wa miili iliyopatikana linaendelea huku pia uokoaji ukiendelea ili kutafuta wengine ambao hawajapatikana.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.