Sunday, August 19, 2018

YANGA WAICHAPA USM ALGER 2 -1

  Malunde       Sunday, August 19, 2018
Club ya Dar es Salaam Young Africans licha ya kuondolewa katika michuano ya Kombe la shirikisho Afrika ikiwa na michezo miwili mkononi ya kukamilisha ratiba, leo imecheza mchezo wake mmoja wa kukamilisha ratiba dhidi ya USM Alger.

Yanga imecheza game yake ya tano ya hatua ya makundi ya michuano ya CAF uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ikiwa ni game yake ya tano ya Kundi D, hiyo ni baada ya kutopata matokeo chanya katika mechi zake nne za mwanzo.
Kwa mara ya kwanza baada ya mechi nne Yanga leo ndio imefanikiwa kuvuna point tatu, baada ya kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-1, magoli ya Yanga yakifungwa na Deus Kaseke dakika ya 43 na Heritier Makambo dakika ya 47, wakati goli la USM Algerlilifungwa na Abdulrahman Meziane dakika ya 52.

Ushindi huo ni wa kwanza kwa Yanga toka mwenyekiti wao Yussuf Manji aonekane leo kwa mara ya kwanza uwanjani na kuwapa hamasa wachezaji, Manji alijiuzulu nafasi hiyo na baadae wapenzi na wanachama walimuomba arudi kuisaidia timu yao inayoaminika kuwa duni kiuchumi kwa sasa.

Yanga iko nafasi ya mwisho Kundi D
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post