Sunday, August 19, 2018

MAN UNITED YAONJA KICHAPO CHA KWANZA EPL

  Malunde       Sunday, August 19, 2018

Wakati Manchester United ikionja kichapo cha kwanza msimu huu baada ya kukubali kufungwa mabao 3-2 na Brighton & Hove Albion, ligi kuu ya soka nchini England EPL imeweka rekodi ya idadi kubwa ya mabao ndani ya siku moja.

Kabla ya Man United kufungwa na Brighton kwa mabao ya Glenn Murray 25', Shane Duffy 27' na Pascal GroƟ 44', EPL ilitanguliwa na ushindi wa majirani zao Manchester City ambao wameilaza 6-1 Huddersfield, hivyo kufanya kupatikana jumla ya mabao 16 ambayo ni idadi kubwa zaidi kwenye siku moja ya EPL ambayo ilihusisha mechi tatu au chini ya hapo.

Ukiacha mabao matano yaliyofungwa kwenye mechi ya Man United na Brighton, mabao mengine manne yamefungwa leo, ambapo Burnley wakiwa nyumbani walikubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Watford. Hivyo ukijumlisha mabao yote katika mechi tatu za leo jumla yake ni 16.

Mbali na rekodi hiyo ya mabao pia Man United imeruhusu kwa mara ya 10 kufungwa goli 3 katika kipindi cha kwanza kwenye historia yake ya kucheza EPL. Mara ya mwisho kufungwa hivyo katika miaka ya hivi karibuni ilikuwa ni mwezi October 2015 kwenye mechi dhidi ya Arsenal.

Kwa upande wake Romelu Lukaku ambaye alifunga bao la kwanza la Man United dakika ya 34 kabla ya Paul Pogba kufunga la pili dakika ya 90, sasa amezifunga timu 18 zinazocheza EPL msimu huu akifanya hivyo kwa misimu tofauti. Timu mbili pekee kati ya 20 ambazo hajazifunga ni Cardiff City na Wolverhampton.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post