KIGOGO WA TFF AFUNGIWA MAISHA KUJIHUSISHA NA SOKA TANZANIAKamati ya Maadili iliyokutana Jumamosi Agosti 25,2018 Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) imemfungia kutojishughulisha na soka Mbasha Matutu.

Matutu ambaye ni Msimamizi wa kituo cha Shinyanga na Mjumbe wa Kamati kuu TFF, amefungiwa kwa makosa matatu ya kushindwa kutekeleza majukumu yake, ubadhirifu, kughushi na kuiba kinyume na kanuni za Maadili na Ligi Kuu.

Kiongozi huyo kwa sasa amefutwa rasmi wadhifa wake ndani ya Shirikisho hilo akiwa kama Mjumbe wa Kamati Kuu na sasa hatohusika tena na masuala ya soka nchini.

Maamuzi hayo yametolewa na TFF kupitia Makao yake yake yaliyopo Ilala, Karume baada ya kuitisha kikao na Waandishi wa Habari.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.