SUMAYE : WAITARA AMEWADHARAU KUPITA KIASI WANA UKONGA

Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye, amesema Mwita Waitara aliyehama Chadema na kuhamia CCM, amewadharau wana Ukonga.

Sumaye ameyasema hayo jana Agosti 25 katika uzinduzi wa kampeni za Chadema, jimbo la Ukonga.

Asia Msangi, ndiye mgombea ubunge jimbo hilo kupitia Chadema katika uchaguzi utakaofanyika Septemba 16.

“Waitara alikuwa mbunge, leo anazungumza habari za Mbowe. Mbowe ndiyo alimchagua kuwa mbunge? Waitara amewadharau sana, amewadharau wana Ukonga kupita kiasi,” amesema.

“Kwanini mtu afanye madharau ya namna hii na sisi tutake kumfikiria? Haya machama yanayojidai yameleta uhuru yana kiburi hujawahi kuona,” aliongeza

Sumaye ambaye ni mjumbe wa Kamati kuu Ya chama hicho, alisema nchi zote zenye maendeleo ni zile ambazo zimeondoa vyama kongwe.

Kadhalika alisema iwapo nchi haina demokrasia ya kweli ya vyama vingi basi taifa litakuwa na wanyonge, na maskini.

“Sisi wengine tumetoka CCM kule ndio kulikuwa na makulaji, kila kitu kipo safi lakini nikasema raha yangu iko wapi kama watanzania wanateseka. Lazima maslahi ya umma yawe mbele kuliko maslahi binafsi,” amlisema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527