Msanii wa Bongo, Snura Mushi amenusurika katika ajali ya gari. Muimbaji huyo alikuwa ameongozana na madensa wake, aliyetoa taarifa ya ajali hiyo iliyotokea majira ya saa nne usiku na Minu Calypto ambaye anatajwa kuwa mpenzi wa Snura.
Kupitia Instagram ameandika; "Jana mida ya saa nne usiku tulipata ajali mimi na Snura Mushi na ma-dancer wetu wawili pamoja na dereva.. Gari ilipinduka ila tunashukuru Mungu tuko salama.. #WeGood"
Social Plugin