Friday, August 10, 2018

GARI LA MBUNGE WA CHADEMA LAPATA AJALI..DEREVA AFARIKI

  Malunde       Friday, August 10, 2018
Gari la Mbunge wa CHADEMA Lucy Magereri lenye namba za usajili T l348 CSR limepata ajali eneo la Issuna wilaya ya Ikungi mkoani Singida ambapo Dereva aliyefahamika kwa jina la Thomas Maro amepoteza maisha papo hapo.


Ajali hiyo imetoka jana Agosti 9 ambapo ndani ya gari hiyo alikuwepo dereva mwenyewe kwani alikuwa analitoa gari hilo Dodoma kulipeleka Shinyanga ndipo lilipogongana na Fuso lililokuwa linatoka Singida kwenda Dar es Salaam.


Dereva wa Fuso amepata majeraha madogo madogo huku mwili wa marehemu ukihifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Singida.


Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Fuso kuendesha gari upande ambao sio wake, na sasa amekamatwa yupo kituo cha Polisi kwa ajili ya mahojiano.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post