Thursday, August 2, 2018

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU KWA TV ZA HOSPITALI KUONESHA MUZIKI

  Malunde       Thursday, August 2, 2018
Na WAMJW - KAGERA
Naibu Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile amepiga marufuku kwa hospitali na vituo vyote vya kutolea huduma za Afya nchini kuonesha miziki katika maeneo yote yakutolea huduma na kuwataka kuweka jumbe zinazohusu Elimu Afya kwa umma pindi wanapongoja kupata huduma.


Ameyasema hayo jana wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika ukumbi wa halmashauri ya Muleba katika Mkoa wa Kagera.


"Ni marufuku kwa hospital zote kuonesha miziki katika maeneo yote ya utoaji huduma za afya" alisema Dkt Ndugulile.


Pia Dkt. Ndugulile amemwagiza Mganga mkuu wa Wilaya ya Ngara DKt. Revokatus Ndyekobora kuhamasisha wananchi Juu ya umuhimu wa kuudhuria kliniki kwa mama mjamzito walau mara nne ndani ya kipindi chá ujauzito wake na kuhakikisha wanajifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya.


"Tuongeze kasi katika kuhamasisha wakina mama wajawazito kuhudhuria kliniki, na kwenda kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya" alisema Dkt Ndugulile. 


Pia alisema kuwa Serikali inaendelea kuboresha sekta ya Áfya nchini kwa kutoa pesa ya ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za Afya na kuhamasisha ushirikishwaji wa wananchi katika ujenzi wa vituo hivyo (Forced account)


"Miundombinu tunaendelea kuboresha, Mkoa mzima tumeleta shilingi Bilion 5.9 kwaajili ya kuboresha vituo vya Áfya, viwili vikiwa katika Wilaya ya Ngara "alisema Dkt Ndugulile .


Kwa upande mwingine Dkt Ndugulile aliendelea kusema kuwa katika kuelekea kuboresha huduma za afya Serikali imeanzasha utaratibu wa kituo nyota kwa vituo vya Áfya, hospitali na Zahanati, na kutoa maagizo kwa Halmashauri zote nchini kuhakikisha Asilimia 80 ya vituo vyake vyote vya kutolea huduma za Afya havishuki chini ya nyota tatu (3)


"Serikali imeanzisha utaratibu wa kutoa madaraja ya Ubora kwa vituo vyote vya kutolea huduma za Afya , tunaanzia nyota sifuri kwa maana Kwamba kiwango chako chá Ubora ni chá chini sana Mpaka nyota 5 ambacho kiwango chako ni chá juu sana, tunataka Asilimia 80 ya Vituo vyao vyote katika kila halmashauri visipungue nyota tatu" Alisema Dkt Ndugulile.


Mbali na hayo Dkt Ndugulile amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Ngara. Luten.... Kuimarisha usimamizi katika ngazi zote za Wilaya ili kuweza kufikia Ubora wa huduma za afya kwa Asilimia 80 katika vituo vyake vyote.


Nae Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ngara Dkt Revokatus Ndyekobora amesema kuwa lishe duni kwa watoto hasa walio chini ya Miaka 5 bado imekuwa tatizo na kusema kuwa wameweka mikakati thabiti yakuweza kupambana dhidi ya tatizo lá lishe duni. 


"Hali ya Lishe bado ni shida, ambapo tunaendelea kupambana nayo na tayari tumeweka mikakati thabiti yakuweza kupambana dhidi ya lishe duni " alisema


DKt. Revokatus Ndyekobora aliendelea kusema kuwa Wilaya ya Ngara ináupungufu wa watumishi kwa Asilimia 59.2 jambo linaloleta changamoto katika utoaji wa huduma za afya.


"Tuna upungufu wa watumishi kwa Asilimia 59.2 , Kwaiyo tunafanya kazi katika hali ya upungufu, tunamshukuru tumepata watumishi 36, lakini waliripoti 33, na juzi TAMISEMI waliondoa watumishi 2" alisema Dkt Revokatus Ndyekobora
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post