SBL YATANGAZA NEEMA KWA WAKULIMA NCHINI


Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Helene Weesie akiwasilisha mada kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira walipotembelea kliwanda cha Dar es Salaam jana
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira wakifuatilia kwa makini mada kutoka kwa Mkurungezi mtendaji wa SBL Helene Weesie walipotembelea kiwanda hicho mapema jana.
Mkurugenzi wa mahusiano wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) John Wanyancha akiwasilisha mada kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira walipotembelea kliwanda cha Dar es Salaam Marema jana
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Saddiq Murad akizungumz a Katika Kikao walipotembelea kiwanda cha Bia cha serengeti (SBL) mara baada ya kutembelea kiranda hicho.

Dar es Salaam, Agosti  15, 2018– Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imetangaza  kutanua mpango wake wa kununua mali ghafi inazotumia kutengenezea bia kutoka kwa wakulima wa ndani kufikia tani zaidi ya tani 17 kufikia mwaka 2020.
Mpango huu ni sehemu ya mkakati wa upanuzi wa uzalishaji wa bia unaofanywa na kampuni hiyo. SBL itanunua mazao yakiwamo mtama
Kwa sasa SBL inanunua tani 15,300 za mazao mbali mbali kutoka kwa mtandao wa wakulima 400 wa ndani kiasi ambacho ni sawa na asilimia 68 ya mahitaji yake kwa mwaka, kwa mujibu wa Mkurugenzi wake Mtendaji  Helene Weesie.
Akiongea na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira waliotembelea kiwanda cha Dar es Salaam jana, Weesie alisema SBL ina mpango wa kutanua mpango huo na kuwafikai wakulima zaidi ya 450, hatua ambayo itawafaidisha wakulima zaidi na kuchangia ukuwaji wa kilimo.
Mpoango wa kuwasidia wakulima unawawezesha wakulima kupata mbegu bora bila malipo, kuwaunganisha na taasisi za fedha kwa ajili ya kupata mikopo ya kupanua kilimo chao pamoja na kuwaunganisha na huduma za ughani. SBL huwahakikishia soko la uhakika kwa kununua mazao yote wanaozalisha
Zaidi ya nusu ya vint=ywaji vinavyozalishwa na SBL ikiwa ni pamoja naPilsner Lager, Kibo Gold, Pilsner King and Senator Lager zinatengenezwa kwa malighafi zinazozalishwa ndani kwa aslimia 100,” anasema Weesie
Kwa kuendelea kutobadilisha tozo la ushuru, Serikali imetuwezesha kutopandisha bei za bia na kuzidisha mapato tunayoyalipa kupitia kodi,”
Mkurugenzi huyo alionya kuwa, kuongezeka kwa kodi kwenye bia kutaathiri mauzo na kuchochea biashara ya pombe haramu.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati hiyo Saddiq Murad alisifia SBL kwa mchango inayotoa kwenye sekta ya viwanda na kuelezea uhu,mimu wa Serikali katika kutengeneza mazingira rafiki  kwa sekta binafsi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527