Thursday, August 16, 2018

MALKIA WA SOUL AFARIKI DUNIA

  Malunde       Thursday, August 16, 2018

Malkia wa muziki wa aina ya 'soul', Aretha Louise Franklin

Malkia wa muziki wa aina ya 'soul', Aretha Louise Franklin kutoka nchini Marekani amefariki dunia hii leo akiwa na umri wa miaka 76, kutokana na ugonjwa uliokuwa unamsumbua wa saratasi.

Aretha ambaye ni mama wa watoto wa nne, amezaliwa mnamo Machi 25, mwaka 1942 ambapo alianza kujihusisha na masuala ya muziki kipindi alipokuwa anaimba injili katika kanisa la New Bethel Baptist lilipo Detroit mjini Michigan nchini humo.

Alipofikisha umri wa miaka 14 aliingia studio kwa mara ya kwanza kwa lengo la kurekodi muziki wake, lakini kwa bahati nzuri kipaji chake cha kuimba hakikuweza kufichika na hatimaye aliweza kuingia mkataba na moja kati ya 'lebel' kubwa za muziki duniani Atlantic Records mnamo mwaka 1966.

Mwaka 1968, alijipatia umaarufu mkubwa barani Ulaya na Marekani akifahamika kama 'Lady Soul' ambapo pia mwaka huo huo alitokea kwenye jarida la Time na kutunukiwa tuzo maalum na kiongozi wa harkati za watu weusi Martin Luther King.

Katika miaka ya 80, Aretha alitoa vibao vikali kama 'who's zooming who' na kile alichoimba na mwanamuziki wa Uingereza George Michael kiitwacho, 'i Knew you were waiting (For Me).

Mwaka 2005, alitunukiwa tuzo ya 'Presidential Medal of Freedom' na Rais George W Bush, kutokana na ushawishi wake kwa mamilioni ya wamarekani.

Katika maisha yake ya muziki, Aretha alifanikiwa kunyakua tuzo 18 za Grammy pamoja na kuwa mwanamke wa kwanza kupewa heshima ya kuwa kwenye orodha ya 'Rock And Roll Hall of Fame'.

Novemba mwaka 2017, Aretha alifanya tamasha lake la mwisho la burudani lililokuwa lenye lengo ya kuchagia mfuko wa Ukimwi wa mwanamuziki wa nchini Uingereza Sir. Elton John.

Wanamuziki wengi duniani wametuma salaam zao za rambirambi wakiongozwa na Sir Elton John, ambaye kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika; 'kifo cha Aretha Franklin ni pigo kwa kila mtu anayependa muziki, pole nyingi kwa ndugu, rafiki na jamaa'.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post