ROMA MKATOLIKI AWACHANA BASATA...."MNAUA SANAA,UBUNIFU NA VIPAJI"


Rapa Roma Mkatoliki ameamua kuwachana Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) huku akidai kuwa taasisi hiyo inaua sanaa, ubunifu na vipaji vya Watanzania.

Roma kupitia ukurasa wake wa Twitter amefunguka hayo na kuwaomba Watanzania waeleze makosa yanayopatikana kwenye wimbo wao mpya na Stamina wa Parapanda.

“BASATA You Are Killing 1. An Art 2. Creativity 3.Talent I don’t Hate The Industry I hate The System!! Hivi Wimbo Wa PARAPANDA Una Matatizo Gani??? Hebu Nisaidie Wewe Mtanzania Mwenzangu!!!!”ameeleza Roma Mkatoliki.

Jana Agosti 6, 2018 Roma na Stamina waliitwa BASATA ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa BASATA alisema waliwatembelea tu kujua Sheria na kanuni mpya za baraza hilo.

Theme images by rion819. Powered by Blogger.