Rais John Magufuli amewasili jijini Mwanza leo Jumamosi Agosti 18, 2018 kwa ndege ya Dreamliner akitokea jijini Dar es Salaam.
Katika safari hiyo kiongozi mkuu huyo wa nchi alizungumza na abiria waliopanda ndege hiyo na kupiga nao picha mbalimbali.
Baada ya kuwasili, Rais Magufuli alikwenda katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando akapopokewa na viongozi kadhaa akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.
Wakati akitoka katika hospitali hiyo alisimamisha msafara wake na kuzungumza na wanafunzi wa Shule Msingi Mongella iliyopo eneo la Bugando waliokuwa wamesimama pembeni mwa barabara.
"Mmekuja kufanya nini hapa," Rais Magufuli aliwauliza swali wanafunzi hao.
Kwa sauti ya pamoja, wanafunzi hao wakajibu "Tumekuja kukuona"
Baada ya jibu hilo, Rais Magufuli aliwashukuru wanafunzi hao na kuwaambia, "Nitarudi siku nyingine kuonana na kuzungumza nanyi. Leo nimefika hapa kumuona mgonjwa wangu ambaye amelazwa hapa hospitalini. Endeleeni kuwaombea wagonjwa waliolazwa hospitalini.”
Baada ya kumaliza kuzungumza na watoto hao aliondoka eneo hilo.
Na Jesse Mikofu, Mwananchi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli akiwasalimia abiria ndani ya ndege Boeing 787-8 Dream Liner ya shirika la ndege la Tanzania (ATCL)alipokuwa akielekea Jijini Mwanza ikiwa ni mara ya kwanza kwa Rais kusafiri kwa kutumia ndege hiyo mpya akiwa na abiria wengine.Agosti 18,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli akiwa amemshika mtoto Ikrama Mahadi(Miezi-3) alipokuwa akiwasalimia abiria ndani ya ndege Boeing 787-8 Dream Liner ya shirika la ndege la Tanzania (ATCL)alipokuwa akielekea Jijini Mwanza ikiwa ni mara ya kwanza kwa Rais kusafiri kwa kutumia ndege hiyo mpya akiwa na abiria wengine.Agosti 18,2018.

Social Plugin