Kituo
cha Sheria na Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Centre -LHRC) kimeendesha mafunzo kwa waandishi wa
habari wilaya ya Shinyanga yaliyolenga kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya haki
za binadamu,jinsia na UKIMWI pamoja na maadili ya uandishi wa habari.
Mafunzo
hayo ya siku mbili yaliyofanyika Agosti 27,2018 na Agosti 28,2018 yamefanyika
katika ukumbi wa Shinyanga Fairies Motel Mjini Shinyanga.
Akifungua
Mafunzo hayo,Mwanasheria kutoka LHRC Theresia Kinabo alisema mafunzo hayo kwa
waandishi wa habari za jamii yatawasaidia kuwajengea uwezo kuhusu haki za
binadamu lakini pia namna ya kuandika habari kuhusu ukatili wa kijinsia na
UKIMWI.
“Mafunzo
haya ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wetu wa Dreams Innovation Challenge, kwa
upande wa waandishi umelenga zaidi kuwawezesha waandishi wa habari kuandika
habari zitakazolisaidia kundi la wasichana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24
waepukane na maambukizi ya VVU”,alisema.
“Mafunzo
haya pia yemetolewa kwa makundi mengine muhimu yanayodili na shughuli za watoto
ikiwemo vyombo vya dola (Dawati la jinsia polisi), mahakama na watu wa afya,viongozi
wa serikali za mitaa ambao wote kwa pamoja wakitimiza wajibu wao watalisaidia
kundi hili la wasichana lenye hatari ya kupata maambukizi ya VVU,” aliongeza Kinabo.
Alisema
kwa mujibu wa takwimu inaonekana katika eneo la Sahara ya Afrika asilimia 71 ya
watoto wanapata maambukizi ya VVU kila siku na chanzo chake ni kufanya mambo
kwa kujaribu lakini pia ikiwemo ndoa katika umri mdogo.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO YALIYOJIRI WAKATI WA MAFUNZO HAYO SIKU YA KWANZA NA YA PILI
SIKU YA KWANZA
Mwanasheria kutoka LHRC Theresia Kinabo akifungua mafunzo mafunzo kwa waandishi wa habari wilaya ya Shinyanga yaliyolenga kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya haki za binadamu,jinsia na UKIMWI na maadili ya uandishi wa habari- Picha zote na Kadama Malunde & Michael Mallya
Mwanasheria kutoka LHRC Theresia Kinabo akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Mwanasheria kutoka LHRC Theresia Kinabo akitoa mada kuhusu haki za binadamu
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwanasheria kutoka LHRC Theresia Kinabo
Waandishi wa habari wakifurahia jambo ukumbini
Mwanasheria kutoka LHRC Getrude Dyabene akielezea kuhusu mradi wa Dreams Innovation Challenge
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini
Waandishi wa habari wakifuatilia mada ukumbini
Mafunzo yanaendelea
Mwezeshaji akitoa mada kuhusu UKIMWI
Waandishi wa habari wakiandika dondoo muhimu
Waandishi wa habari wakiandika dondoo muhimu
Waandishi wa habari wakifuatilia mada ukumbini
ANGALIA PICHA SIKU YA PILI YA SEMINA
Afisa Mawasiliano kutoka LHRC Michael Mallya akitoa mada kuhusu maadili ya uandishi wa habari katika kuandika habari zinazohusu VVU na UKIMWI
Afisa Mawasiliano kutoka LHRC Michael Mallya akiendelea kutoa mada
Afisa Mawasiliano kutoka LHRC Michael Mallya akiendelea kutoa mada wakati wa mafunzo hayo
Mwanasheria kutoka LHRC Theresia Kinabo akitoa mada kuhusu Ukatili wa kijinsia
Mwanasheria kutoka LHRC Theresia Kinabo akisisitiza jambo ukumbini
Mwanasheria kutoka LHRC Theresia Kinabo akielezea nafasi ya waandishi wa habari katika kupiga vita ukatili wa kijinsia
Mmiliki wa Malunde1 blog,Kadama Malunde akiwa ukumbini
Mwanasheria kutoka LHRC Getrude Dyabene akielezea kuhusu Sheria ya kudhibiti na kupambana na UKIMWI
Mwanasheria kutoka LHRC Getrude Dyabene akifafanua kuhusu haki ya afya
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini
Waandishi wa habari wakifuatilia mada ukumbini
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini
Social Plugin