NAIBU MEYA DAR,MWANASHERIA MKUU WA CUF WAJIUZULU

Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mussa Swedi Kafana Diwani wa Kiwalani na Mwanasheria Mkuu wa CUF - Maalim, Hashim Bakari Mziray wamejiuzulu uanachama CUF pamoja na nyadhifa zao zote na kujiunga CCM. 


Wamedai kuwa, wameamua kuhama kutokana na Viongozi wa upinzani kuonyesha unafiki na kushindwa kushirikiana.


“Chama cha CUF kina pande mbili zinavutana, na mgogoro huu hauwezi kuisha leo wala kesho kwasababu wanaobishana na kuvutana ni watu wakubwa kwenye chama” amesema Kaffana na kuongeza;

"Migogoro ya chama cha CUF inaweza kuniharibia future yangu kisiasa na uongozi kwa ujumla hivyo kwa dhati ya moyo wangu pasipo kushawishiwa na mtu yoyote ninajivua uanachama na kuachia madaraka ya unaibu meya wa jiji la Dar es salaam pamoja na udiwani"

Kwa upande wake alieykuwa Mwanasheria Mkuu wa chama hicho na Wakili wa Mahakama Kuu, Bwana Hashim Mziray amesema kuwa migongano ya pande mbili ndani ya chama hicho imemfanya aachie nafasi zake hizo huku akitaka kujiunga na CCM akidai ndio chama chenye mwelekeo wa kuwaletea maendeleo wananchi wake kupitia kwa Mwenyekiti wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Na Magdalena Kashindye
Theme images by rion819. Powered by Blogger.