MWANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE AKUTWA AMEFARIKI

Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Old Tanga, Shufaa Mbughuni amekutwa amefariki dunia huku uso wake ukiwa umechubuliwa ngozi.


Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Tanga, Edward Bukombe amesema mwili wa mwanafunzi huyo umekutwa jana Agosti 19, 2018 saa 9.40 alasiri katika mtaa wa Majani Mapana kata ya Nguvumali jijini Tanga.

Bukombe alisema taarifa kamili kuhusiana na tukio hilo ataitoa mara baada ya madaktari wa hospitali ya mkoa wa Tanga ya Bombo kuufanyia uchunguzi mwili wa mwanafunzi huyo.

Naye baba wa mwanafunzi huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Majani Mapana, Salim Mbughuni amesema mwanaye aliwaaga wenzake juzi saa 2.00 usiku kwamba anakwenda kijisomea lakini hakurudi kama ilivyo kawaida yake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527