Tuesday, August 28, 2018

MBASHA MATUTU AKUBALI YAISHE KIFUNGO CHA MAISHA SOKA KILICHOTOLEWA NA TFF

  Malunde       Tuesday, August 28, 2018
Aliyekuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF kutoka Mkoani Shinyanga Mbasha Matutu amekubali kujiweka pembeni kutokujihusisha na suala la soka hapa nchini kutokana na adhabu aliyopewa na kamati ya maadili ya TFF chini ya Mwenyekiti wa kamati Wakili Hamidu Mbwezeleni.

Akizungumza na Famara News na Famara Tv Mbasha amesema amefurahi kwa kupunguziwa majukumu yake aliyokuwa anayafanya katika soka nchini na kwa sasa anajikita katika kuendeleza mambo yake ya kimaendeleo.

Matutu amesema tuhuma ambazo amehukumiwa nazo hazina msingi maana maana viongozi mbalimbali walikuwepo kwenye mchezo baina ya Simba na Stand United, Viongozi kutoka TFF, kutoka Bodi ya Ligi na Kutoka FA mkoa wa Shinyanga.

Matutu ameiasa TFF kuacha siasa za kuwaondoa watu ambao hawawataki kwenye listi yao ila wajenge taasisi mahiri na yenye nguvu katika kuendeleza soka hapa nchini maana TFF sio mali ya mtu ila mali ya UMMA.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili Wakili Hamidu Mbwezeleni alisema kamati imeshafanya maamuzi yake na yeye kama msemaji wake hawezi kuendelea kuzungumzia kitu hicho zaidi ya kutafuta nakala ya hukumu na kuisoma. 

Aidha alionyesha kuhamaki alipoulizwa kwanini hataki kuzungumza wakati ndio amepewa nafasi ya kuzungumza katika mambo ya kamati ya maadili, Wakali Mbwezeleni alisema hawezi kuzungumzia mambo ya udaku.

Mbasha Matutu anakuwa kiongozi wa pili kuhukumiwa kifungo cha maisha cha kutokujihusisha na masuala ya soka, akitanguliwa na Michael Wambura ambaye alikuwa Makamu Rais wa TFF. Makosa wa Mbasha Matutu ni kudanganya hesabu ya mapato ya mechi baina ya Stand United na Simba Uwanja wa Kambarage Shinyanga.

Nani atafuata kwenye list ya kufungiwa na TFF, ni suala la kusubiri na kulipa muda.
Fabian Fanuel @FMG
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post