MAN UNITED YAICHAPA LEICESTER 2 - 0 YAACHA REKODI


Wachezaji wa Man United wakishangilia bao la pili dhidi ya Leicester City.

Klabu ya soka ya Manchester United imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Leicester City kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi kuu ya soka nchini England katika msimu wa 2018/19 iliyomalizika usiku huu wa Agosti 10, 2018 kwenye uwanja wa Old Trafford.

Mabao ya Manchester United katika mchezo huo ambao umeacha rekodi mbalimbali yamefungwa na Paul Pogba dakika ya 3 kwa penati na Luke Shaw dakika ya 83 huku Jamie Vardy akifunga la Leicester City dakika ya 90+2.

Mchezo huo umewafanya Man United kutopoteza mechi hata moja kati ya 122 za EPL kwenye uwanja wa Old Trafford pale ambapo walianza kutangulia kufunga. Mara ya mwisho kutangulia kufunga kisha wakapoteza ilikuwa ni mwaka 2009 ambapo walipoteza 4-1 dhidi ya Liverpool.

Pia kocha Jose Mourinho ameweka rekodi ya kutopoteza mechi katika michezo yake 18 ya ufunguzi wa ligi katika maisha yake ya ukocha. Ameshinda mechi 9 kati ya 10 za ufunguzi kwenye EPL pekee ambako pia ametoa sare 1. Naye Luke Shaw amefunga bao lake la kwanza ndani ya United ikiwa imemchukua mechi 67 katika mashindano yote.

Kwa upande wao Leicester City wameweka rekodi mbovu ya kuwa timu ya kwanza kufungwa bao la kwanza la msimu kwenye ligi kuu ya England ndani ya misimu mitatu mfululizo ya hivi karibuni.

Pia hii imekuwa ni mara ya pili katika historia ya ligi kuu ya England mechi ya ufunguzi kuchezwa Ijumaa na mechi zote Leicester City imecheza na kupoteza. Mara ya kwanza ilikuwa msimu uliopita ambapo ilikubali kichapo cha mabao 4-3 kutoka kwa Arsenal


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527