Sunday, August 19, 2018

MADAKTARI WAJITOLEA KUOKOA MAISHA YA MBUNGE BOBI WINE

  Malunde       Sunday, August 19, 2018

Mbunge wa Kyadondo Mashariki, nchini Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu 'Bobi Wine'.

Mbunge wa Kyadondo Mashariki, nchini Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu 'Bobi Wine' amepata matatizo ya figo na inaelekea kutokufanya kazi.

Hii ni kwa mujibu wa Mawakili wake waliokwenda kumtembelea Mbuge huyo katika Kambi ya Jeshi ya Makindye anakoshikiliwa

Kwa mujibu wa gazeti la Uganda la Daily Monitor, Madaktari hao hii leo kupitia Chama cha Madaktari nchini humo, (UMA), wako tayari kumpatia Mbunge huyo matibabu ya kitaalam ya hali ya juu ambaye sasa inaelezwa anapigania maisha yake katika kambi hiyo ya kijeshi.

Madkatari hao wametoa ombi hilo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mawakili wa Bobi Wine, wakisema mteja wao anahitaj haraka matibabu ya kitaalam ili kuokoa maisha yake.

Hata hivyo wamesema hawawezi kutekeleza matibabu hayo bila kupata idhini kutoka Serikalini, kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Rais wa UMA, Dk. Ekwaro Obuku.

Hayo yanajiri ikiwa ni siku chache tangu dereva wa Bobi Wine, kuuawa kwa kupigwa risasi katika vurugu wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Arua .

Staa wa muziki nchini Uganda, Jose Chameleone amemuandikia barua ya wazi Rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni kwa lengo la kumuombea msamaha msanii mwenzake huyo ambaye anashikiliwa na Jeshi la Polisi hadi hivi sasa kwa tuhuma za uchochezi.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post