RAIS WA VENEZUELA ANUSURIKA KUUAWA

RAIS wa Venezuela, Nicolas Maduro, ameapa kuhakikisha kuwa sheria inachukua mkondo wake baada ya jaribio linalodaiwa kufanyika dhidi ya maisha yake ambalo anasema limepangwa na rais wa Colombia Juan Manuel Santos.

Ndege zisizokuwa na rubani zikiwa na milipuko zililipuka karibu na rais huyo katika jaribio la kutaka kumuua ambalo lilitokea wakati akitoa hotuba kwa maelfu ya wanajeshi ambayo ilikuwa inatangazwa moja kwa moja katika televisheni.

“Hili lilikuwa jaribio la kutaka kuniua,” alisema baadaye alipolielezea tukio hilo. “Leo walijaribu kuniua.”

Waziri wa Habari, Jorge Rodriguez, alisema tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya saa 11.30 jioni saa za Venezuela wakati Maduro alikuwa akisherehekea siku ya jeshi la taifa. 


Kiongozi huyo ambaye alionekana dhahiri kuingiwa woga alisema aliona “kitu kinaruka angani ” ambacho kililipuka mbele ya macho yake. Alidhani huenda ni kitu kilichokuwa kimelengwa kwa ajili ya maonyesho kwa heshima ya sherehe hiyo.

Katika muda wa sekunde kadhaa, Maduro alisema alisikia mlipuko wa pili na mtafaruku ulifuatia. Walinzi wake walimuondoa Maduro kutoka katika mahali hapo na picha za televisheni zilionyesha wanajeshi waliokuwa katika sare za jeshi walioikuwa wamesimama katika utaratibu fulani haraka wakitawanyika kutoka katika eneo hilo.

Alisema , “kundi la mrengo wa kulia” likifanya kazi kwa uratibu na wapinzani mjini Bogota na Miami, ikiwa ni pamoja na Rais wa Colombia, Juan Mnuel Santos, wanahusika. 

Baadhi ya “wale waliotoa baadhi ya vifaa ” vilivyotumika katika shambulio hilo tayari wameshakamatwa akiongoza uhunguzi utafanyika kubaini kiini cha shambulio hilo bila kujali nani atahusika

Kundi lisilojulikana la waasi ambalo linaundwa na raia wa Venezuela na wanajeshi lilidai kuhusika na shambulio hilo la kutaka kumuua Maduro, hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa katika mtandao wa kijamii.

“Ni kinyume na hadhi ya jeshi kuwalinda watu katika serikali ambao hawakusahau tu katiba , lakini pia ambao wamefanya ofisi za umma kuwa ni fursa ya kujitajirisha,” kundi hilo limesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527