Tuesday, August 7, 2018

WAZIRI KIGWANGALLA AFUNGUKIA KITANDANI " SIJUI HATA KWANINI USIKU HUU NIMEGUSA SIMU??

  Malunde       Tuesday, August 7, 2018

August 4, 2018 Waziri wa Maliasili na Utalii Dr. Hamisi Kigwangalla alipata ajali ya gari akitokea Arusha kabla ya kufika katika eneo la Magugu na hali yake ilikuwa mbaya na baadae kuchukuliwa na Helicopter na kuhamishiwa hospitali ya Mount Meru na baadae Muhimbili.


Katika ajali hiyo ilipoteza maisha ya mwandishi wa habari na mpiga picha wa waziri Kingwalla aliyekuwa anajulikana kwa jina la Hamza Temba, usiku wa August 7,2018 waziri Kigwangalla ameonesha dalili za kuwa anaendelea vizuri baada ya kutumia simu yake kupost instagram na facebook ujumbe unaoeleza.

Citizensfor Kigwangalla is at Muhimbili National Hospital.
Sijui hata Kwa nini usiku huu nimegusa simu? 😭😭😭 Only to learn the reality that mdogo wangu, bwashee wangu, this hard working, smart, handsome and very hopeful young man is no more! What more can I say?! Alhamdulillah. Qaalu inna lillah wainna ilayhir rajiuun. 🙏🏿

Citizensfor Kigwangalla is at Dar es Salaam.
Its my 43rd birthday today, alhamdulillah. Ahsante Allah kwa kunifikisha leo hii. Mimi ni shuhuda wa nguvu zako na upendo wako. Hakika wewe ni Mkuu, ni mwema sana. Ni mwenye huruma sana. Ni mwenye kusamehe sana. Ni mwenye kurehemu neema kubwa kubwa na neema ndogo ndogo. Umenipa mtihani na funzo kubwa sana kwenye maisha yangu. Naomba uendelee kunipa ulinzi wako. Unijaalie maisha mema marefu yenye faida kwangu na kwa viumbe wako. Nakushukuru kwa hali hii na ninajua utaniafu mapema ili nizidi kuutangaza ukuu na utukufu wako ya Allah. Kwa uamuzi na kwa uweza wako hakuna kinachoshindikana ya Allah. Wewe ndiyo kila kitu. Ninakuomba siha, furaha na mafanikio tele kwa familia yangu, ndugu, jamaa, viongozi wakuu wangu, viongozi wenzangu, marafiki na wananchi wenzangu wote wanaoniombea dua. Kwa wapiga kura wenzangu wa Nzega, poleni, nilikuwa nakuja ziara yetu ya jimbo ndo nikapata ajali hii; mzidi kuniombea dua ili nipone haraka niendelee kuwatumikia. Kwa sasa Naendelea vizuri, alhamdulillah, japo nina maumivu makali sana. #AllahAkbar
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post