JAMAA AJITEKA MWANZA AKITAKA ATUMIWE PESA

Jeshi la Polisi Mwanza limemkamata Prosper Lema umri miaka 26, Mchaga kwa kosa la kujiteka kisha kutuma ujumbe kwa ndugu zake akitaka atumiwe pesa kiasi cha Milioni 5.3, ili aongeze mtaji wake wa vileo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, amesema, taarifa hizo za Bw. Lema zilipatikana baada ya ndugu zake mtuhumiwa huyo kwenda katika kituo cha polisi kirumba jijini humo kutoa taarifa ya ndugu yao kutekwa na watu wasiojulikana Julai 18, mwaka huu baada ya kuwatumia ujumbe akiomba fedha.

Kamanda Msangi amesema kwamba mtuhumiwa Lema aliomba fedha zaidi ya shilingi milioni tano kwa familia yake kwa kutuma ujumbe kwenye simu ili aweze kuachiwa huru na watu waliomteka.

Aidha ameongeza kwamba mtuhumiwa Lema atafikishwa Mahakamani pindi uchunguzi wa tukio hilo utakapokamilika.

Mbali na hayo, Kamanda Msangi amewatahadharisha wananchi kuwa makini na kutoa taarifa kwa vyombo vya dola pindi wanapobaini kuwepo kwa dalili zinazofanana na hizo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527