HAWA GHASIA AJIUZULU

 Mbunge wa Kibakwe (CCM), George Simbachawene amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya bajeti leo Jumanne Agosti 28, 2018.

Katika uchaguzi huo, mbunge wa Maswa Magharibi (CCM), Mashimba Ndaki amechaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa kamati hiyo.

Uchaguzi wa viongozi wa kamati hiyo umefanyika baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti wa kamati hiyo, Hawa Ghasia na makamu wake, Jitu Soni.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo, Simbachawene amesema mapema leo alihamishwa kutoka kamati ya Bunge ya katiba na sheria kwenda kamati ya bajeti.

Amesema baada ya kuhamishwa na kukuta nafasi ipo wazi, aliamua kugombea uenyekiti na kushinda kwa kishindo.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.