CHADEMA YATEUA WAGOMBEA UBUNGE,UKONGA,KOROGWE VIJIJINI NA MONDULI

Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), kimetangaza majina ya wagombea wake watakaowania ubunge katika majimbo ya Ukonga, Korogwe Vijijini na Monduli kupitia kikao cha kamati kuu ya chama.



Katibu wa chama hicho kanda ya kaskazini Amani Golugwa amesema kuwa tayari chama hicho kupitia mkutano wake kimekwisha pitisha majina ya watakaopeperusha bendera za chama hicho katika uchaguzi mdogo wa Septemba 16, 2018.


Golugwa amewataja wagombea hao kuwa ni Amina Ally atakayegombea ubunge jimbo la Korogwe Vijijini, aliyekuwa Diwani wa kata ya Lepurko Yonas Masiaya Laizer atasimama jimbo la Mondulipamoja na Asia Msangi atakayeiwakilisha Chadema jimbo la Ukongajijini Dar es salaam.


Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika majimbo matatu na wa udiwani katika kata mbili za Tanzania Bara utakaofanyika Septemba 16, mwaka huu.



Uchaguzi huo utafanyika ikiwa ni mwezi mmoja kupita tangu ufanyike uchaguzi mwingine mdogo katika jimbo la Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma pamoja na kata 79 nchini ambapo Chama cha Mapinduzi (CCM) kilishinda kwa asilimia 100%.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527