Monday, August 27, 2018

BOBI WINE AACHIWA KWA DHAMANA KESI YA UHAINI UGANDA

  Malunde       Monday, August 27, 2018

Bobi Wine akiwa mahakamani.

Mahakama Kuu ya Gulu nchini Uganda imempatia dhamana Mbunge wa Kyadondo Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine katika kesi yake inayomkabili ya uhaini.

Dhamana hiyo ni baada ya Mbunge huyo na wenzake 34 waliofika mahakamani mjini Gulu kuomba mahakama iwaachilie kwa dhamana leo asubuhi wakiwa na mawakili wao.

Jaji wa mahakama ya Gulu Stephen Mubiru alikubali maombi ya dhamana hiyo, baadhi ya watu walioshtakiwa pamoja na mbunge huyo ni Mbunge wa kuteuliwa Kassino Wadri, Mbunge wa Jinja Magharibi,Paul Mwiru,Mbunge wa Ntungamo Gerald Karuhanga, na aliyekuwa mstaafu wa Makindye Mike Mabikke.

Mbunge huyo mpaka kukamatwa kwake na kushikiliwa kwenye gereza la jeshi la Makindye nchini humo alidaiwa kukamatwa akiwa na risasi na kuushambulia msafara wa Rais Yoweri Museveni kwa mawe. Lakini Bobi Wine ameonekana akitembea kwa magongo na kuzua masikitiko kwa wafuasi wake mahakamani hapo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post