Picha : BASI LA SARATOGA LATEKETEA KWA MOTO


Basi la kampuni ya Saratoga lililokuwa likitoka mkoani Kigoma kwenda Sumbawanga limeshika moto na kuteketea lote katika eneo la kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma leo asubuhi. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, ACP Martin Ottieno amesema kuwa jeshi lake bado linachunguza chanzo cha moto huo, ambapo amebainisha kuwa abiria wote sitini wamepona na baadhi ya mizigo imeokolewa. 

“Gari limekaguliwa kabla ya kuondoka katika stendi ya mabasi kama kawaida ya utaratibu wa kikosi cha usalama barabarani na hakuna tatizo lililoonekana, hivyo chanzo cha moto huo bado hakija julikana tunafanya uchunguzi”, amesema Kamanda Ottieno. 

Basi hilo limeungua ikiwa ni siku moja toka mtu mmoja kupoteza maisha katika ajali ya moto ulioteketeza malori katika mpaka wa Tanzania na Rwanda (Rusumo), baada ya gari la mafuta ya petrol kuligonga gari jingine na kupoteza mfumo wa breki.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527