YANGA YAFANYA UTEUZI MRITHI WA CLEMENT SANGA

Mara baada ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Young Africans, Clement Sanga kujiuzulu, Kamati ya Utendaji kwa kushirikiana na Bodi ya Wadhamini wamefanya kikao cha dharula na kumteua kiongozi mwingine atakayeshikilia nafasi hiyo iliyoachwa wazi.


Katika taarifa iliyotolewa jana na Afisa habari Yanga, Dismas Ten amesema Kamati ya Utendaji pamoja na Bodi ya Udhamini imemteua Omary Kaya kuwa Kaimu Katibu Mkuu kwa kipindi hiki cha mpito ili kuweza kurudisha utendaji wa kazi na shughuli za kila siku kwenye klabu.



Aidha amesema zipo nafasi kadhaa ambazo zipo wazi, Kamati ya Utendaji na Bodi ya Udhamini inaendelea kushughulikia taratibu husika za nafasi hizo na muda mfupi ujao itawekwa wazi nani atashika nafasi hizo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527